Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 24 Februari 2026

Utangulizi wa Web3

Uwekaji kati umesaidia mabilioni ya watukwenye wavuti ya ulimwenguni kote na kuunda miundombinu thabiti inayoishi. Wakati huo huo mashirika machache ya jumuiya kuu yana ngome katika maeneo makubwa ya wavuti ya ulimwenguni kote, yenye kuamua kipi kuruhusiwe na kipi kisiruhusiwe.

Tovuti ya tatu ni suluhisho la shida hii. Badala ya mtandao uliohodhiwa na makampuni makubwa ya teknolojia, tovuti ya 3 inakumbatia ugatuaji na inajengwa kuendeshwa na kumilikiwa na watumiaji wake. Tovuti ya tatu inaweka mamlaka au nguvu katika mikono ya watu binafsi badala ya taasisi au mashirika binafsi. Kabla ya kuongelea tovuti ya tatu, tuangalie namna tulivyofika hapa.

Wavuti ya awali

Watu wengi hufikiria mtandao kama nguzo yenye kuendelea ya maisha ya kisasa iligunduliwa na ikawepo tangu wakati huo. Ingawa, mtandao/wavuti wengi wetu tunavyoufahamu sasa ni tofauti na ilivyofikiriwa awali. Ili kuelewa hili vizuri ni vyema ni kuvunja historia fupi ya mtandao/tovuti katika vipindi huru tovuti 1.0 na tovuti 2.0.

Web 1.0: Kusoma Pekee (1990-2004)

Mwaka 1989 huko CERN, Geneva Tim Berner-lee alikuwa bize kutengeneza itifaki ambayo ingekuwa wavuti ya mtandao wa ulimwengu. Wazo lake? Kutengeneza itifaki zilizo wazi zilizoruhusiwa kushiriki taarifa kote ulimwenguni.

Uanzishwaji wa kwanza wa uundaji wa Berners-Lee ambao kwa sasa unajulikana kama 'tovuti 1.0', ulitokea takribani kati ya mwaka 1990 hadi 2004. Tovuti 1.0 ilikuwa tovuti zilizotulia ambazo zilimilikiwa na makampuni, na hakukuwa na muingiliano kati ya watumiaji watu binafsi mara chache walitoa maudhui - na kusababisha kujulikana kama wavuti ya kusoma tu.

Muundo wa mteja-seva, unaowakilisha Web 1.0

Web 2.0: Kusoma-Kuandika (2004-sasa)

Kipindi cha tovuti 2.0 kilianza mnamo mwaka 2004 ikiwa ni pamoja na kuibuka kwa majukwaa ya mitandao ya kijamii. Badala ya Kusoma tu, wavuti hii ilibadilika na kuwa ya kusoma-kuandika. Badala ya makampuni kutoa maudhui kwa watumiaji, walianza pia kutoa majukwaa ya kushiriki maudhui yanayotokana na mtumiaji na kujihusisha na mwingiliano kati ya mtumiaji na mtumiaji. Kadiri watu wengi walivyoingia mtandaoni, makampuni machache maarufu yalianza kudhibiti idadi isiyo na uwiano pamoja na thamani inayozalishwa kwenye wavuti. Tovuti 2.0 pia ilizalisha mtindo wa mapato unaoendeshwa na utangazaji. Ingawa watumiaji wanaweza kuunda maudhui, hawakuyamiliki au kunufaika nayo kutokana na uchumaji wake wa mapato.

Muundo wa mteja-seva, unaowakilisha Web 2.0

Web 3.0: Kusoma-Kuandika-Kumiliki

Dhana ya 'Web 3.0' ilibuniwa na mwanzilishi mwenza wa Ethereum Gavin Wood muda mfupi baada ya Ethereum kuzinduliwa mwaka 2014. Gavin aliweka kwa maneno suluhisho la tatizo ambalo watumiaji wengi wakwanza wa sarafu za kidijitali walihisi: Mtandao ulihitaji uaminifu mkubwa. Huo ni, Mtandao mkubwa ambao watu wanaujua na kutumia leo unategemea kuamini makampuni machache ya kibinafsi kufanya kazi kwa manufaa ya umma.

Muundo wa nodi uliogatuliwa, unaowakilisha Web3

Je, Web3 ni nini?

Tovuti ya tatu imekuwa muda wa kuvutia watu wote kwa maono ya mtandao mpya, bora zaidi. Kwa msingi wake, tovuti ya tatu hutumia mnyororo wa bloku, cryptocurrensets, na NFTs kurejesha nguvu kwa watumiaji katika mfumo wa umiliki. Chapisho la mwaka 2020 kwenye Twitter (opens in a new tab) lilisema vyema zaidi: Web1 ilikuwa ya kusoma-pekee, Web2 ni ya kusoma-kuandika, Web3 itakuwa ya kusoma-kuandika-kumiliki.

Mawazo ya msingi ya Web3

Ingawa ni changamoto kutoa ufafanuzi wa tovuti ya tatu ni nini, kanuni chache za msingi huongoza uundaji wake.

  • Web3 imegatuliwa: badala ya sehemu kubwa za mtandao kudhibitiwa na kumilikiwa na huluki za kati, umiliki unasambazwa miongoni mwa wajenzi na watumiaji wake.
  • Web3 haina ruhusa: kila mtu ana ufikiaji sawa wa kushiriki katika Web3, na hakuna anayetengwa.
  • Web3 ina malipo ya asili: inatumia sarafu ya kidigitali kwa matumizi na kutuma pesa mtandaoni badala ya kutegemea miundombinu iliyopitwa na wakati ya benki na wasindikaji wa malipo.
  • Web3 haiitaji uaminifu: inafanya kazi kwa kutumia vivutio na mifumo ya kiuchumi badala ya kutegemea wahusika wengine wanaoaminika.

Kwanini tovuti ya tatu ni muhimu?

Ingawa vipengele vikuu vya tovuti ya tatu havijatengwa na havitoshi katika kategoria nadhifu, kwa urahisi tumejaribu kuvitenganisha ili kurahisisha kueleweka.

Umiliki

Tovuti ya tatu inakupa umiliki wa mali zako za kidijitali kwa njia ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kwa mfano, unacheza mchezo wa wa tovuti ya pili. Kama ukinunua bidhaa ya ndani ya mchezo, inahusishwa moja kwa moja na akaunti yako. Kama mtengenezaji wa gemu au mchezo akifuta akaunti yako, utapoteza vitu hivi. Au, kama ukiacha kucheza mchezo, utapoteza thamani uliyowekeza kwenye bidhaa zako za ndani ya mchezo.

Web3 inaruhusu umiliki wa moja kwa moja kupitia . Hakuna mtu yeyote, hata watayarishaji wa mchezo, aliye na uwezo wa kukunyang'anya umiliki. Na, kama ukiacha kucheza, unaweza kuuza au kubadilishana bidhaa zako za ndani ya mchezo kwenye soko huria na kurudisha thamani yake. Gundua michezo ya onchain ili kuona hili likifanyika.

Ukinzani dhidi ya udhibiti

Nguvu kubwa inayobadilika kati ya majukwaa na waundaji maudhui haijasawazishwa kwa kiasi kikubwa.

OnlyFans pekee ndio tovuti ya maudhui ya watu wazima inayozalishwa na watumiaji na waundaji maudhui zaidi ya milioni 1, wengi wao wakitumia jukwaa kama chanzo chao kikuu cha mapato. Mnamo Agosti 2021, OnlyFans ilitangaza mipango ya kupiga marufuku maudhui ya ngono waziwazi. Tangazo hilo lilizua hasira miongoni mwa watayarishaji kwenye jukwaa, ambao walihisi kuwa walikuwa wakiibiwa mapato kwenye jukwaa ambalo walisaidia kuunda. Mara baada ya mzozo huo, uamuzi ulibadilishwa haraka. Licha ya waundaji kushinda vita hii, inaonyesha tatizo la waundaji la wavuti ya 2.0: unapoteza sifa na wafuasi uliowapata kwenye jukwaa kama utaondoka.

Kwenye wavuti wa 3, taarifa zako zinaishi kwenye kiambajengo. Ukiamua kuondoka kwenye jukwaa, unaweza chukua sifa zako, ukazieka kwenye kiunganishi kingine kinachoendana na maadili yako.

Wavuti wa 2 inamuhitaji muunda maudhui kuamini jukwa kutokubadilisha sheria zao, lakini kuzuia uthibiti ni kipengele cha asili cha jukwa la wavuti wa 3.

Mashirika huru yaliyogatuliwa (DAOs)

Kama kumiliki taarifa zako kwenye wavuti wa 3, unaweza kumiiki jukwaa kwa ujumla, kwa kutumia tokeni zinazokuwa kama hisa kwenye kampuni. Mashirika gatuzi yanakuwezesha kuendesha umiliki wa jukwaa na kufanya maamuzi kuhusu baadae yake.

DAOs zinafafanuliwa kitaalamu kama iliyokubaliwa ambayo hufanya maamuzi yaliyogatuliwa kiotomatiki juu ya hazina ya rasilimali (tokeni). Watumiaji wenye tokeni wanapiga kura jinsi rasilimali itakavyo tumika, na msimbo automatiki unafanya mrejesho wa kura.

Hata hivyo, watu wengi hueleza jamii nyingi za wavuti wa 3 kama mashirika gatuzi. Jamii hizi zina viwango tofauti vya ugatuzi na automatiki kwa kutumia msimbo. Sasa ivi, tuna chunguza nini ni mashirika gatuzi na jinsi gani yatakavyo kuwepo siku zijazo.

Utambulisho

Kiasilia, ungeunda akaunti kwa kila jukwaa utakalotumia. Kwa mfano, unaweza ukawa na akaunti ya Twitter, akaunti ya YouTube, na akaunti ya Reddit. Unataka kubadilisha uonekanaji wako au wasifu picha? Utatakiwa kufanya kwa kila akaunti. Unaweza kuingia kwa kutumia jamii nyinginezo, lakini hii inaleta shida inayojuliakna ya uthibiti. Kwa kubonyeza mara moja, jukwaa hili linaweza kukufungia nje maisha yako ya mtandaoni. Hata vibaya zaidi, majukwaa mengi yanahitaji uwaamini wao na taarifa za utambulisho binafsi kutengeneza akaunti.

Web3 hutatua matatizo haya kwa kukuruhusu kudhibiti utambulisho wako wa kidijitali na anwani ya Ethereum na wasifu wa . Kutumia anwani ya Ethereum unakuwezesha kuingia kwa mara moja kwenye majukwaa ambayo ni salama, yanazuia uthibiti kutoka kwa mtu mwingine, na kutokujulikana.

Malipo ya asili

Miundombinu ya malipo ya wavuti wa 2 unategemea mabenki na wachakata miamala, ikitoa watu bila akaunti za benki au hao ambao imetokea wanaishi kwenye mipaka ya nchi isiyo sahihi. Web3 hutumia tokeni kama kutuma pesa moja kwa moja kwenye kivinjari na haihitaji mhusika mwingine anayeaminika.

Zaidi kuhusu ETH

Mapungufu ya Web3

Licha ya manufaa mengi ya Web3 katika hali yake ya sasa, bado kuna vikwazo vingi ambavyo mfumo wa ikolojia lazima ushughulikie ili uweze kustawi.

Upatikanaji

Vipengele muhimu vya Web3, kama vile Kuingia kwa kutumia Ethereum, tayari vinapatikana kwa mtu yeyote kutumia kwa gharama sifuri. Lakini, gharama ya miamala bado ni kubwa kwa wengi. Web3 ina uwezekano mdogo wa kutumiwa katika mataifa maskini, yanayoendelea kutokana na ada za juu za ununuzi. Kwenye Ethereum, changamoto hizi zinatatuliwa kupitia ramani na . Teknolojia iko tayari, lakini tunahitaji viwango vya juu zaidi vya kupitishwa kwenye safu ya 2 ili kufanya Web3 ipatikane na kila mtu.

Uzoefu wa mtumiaji

Kizuizi cha kiufundi cha kuingia kwa kutumia Web3 kwa sasa kiko juu sana. Watumiaji lazima waelewe maswala ya usalama, waelewe nyaraka ngumu za kiufundi,, na waelekeze miingiliano ya violesura. Watoa huduma za mkoba, hasa, wanafanya kazi kutatua hili, lakini maendeleo zaidi yanahitajika kabla ya Web3 kupitishwa kwa wingi.

Elimu

Web3 inaleta dhana mpya zinazohitaji kujifunza miundo tofauti ya kiakili kuliko ile inayotumika katika Web2.0. Msukumo kama huo wa elimu ulitokea wakati Web1.0 ilipokuwa ikipata umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990; wafuasi wa wavuti wa ulimwengu mzima walitumia mbinu nyingi za kielimu kuelimisha umma kutoka kwa sitiari rahisi (barabara kuu ya habari, vivinjari, kuvinjari wavuti) hadi matangazo ya televisheni (opens in a new tab). Web3 sio ngumu, lakini ni tofauti. Mipango ya kielimu kuwafahamisha watumiaji wa Web2 kuhusu dhana hizi za Web3 ni muhimu kwa mafanikio yake.

Ethereum.org inachangia elimu ya Web3 kupitia Programu yetu ya Tafsiri, ikilenga kutafsiri maudhui muhimu ya Ethereum katika lugha nyingi iwezekanavyo.

Miundombinu ya kati

Mfumo ikolojia wa Web3 ni mchanga na unabadilika haraka. Kama matokeo, kwa sasa inategemea sana miundombinu ya mfumo mkusanyo (GitHub, Twitter, Discord, nk). Makampuni mengi ya Web3 yanaharakisha kujaza mapengo haya, lakini kujenga miundombinu ya ubora wa juu na ya kuaminika inachukua muda.

Mustakabali uliogatuliwa

Web3 ni mfumo mchanga na unaoendelea. Gavin Wood aliunda neno hilo mnamo 2014, lakini mengi ya maoni haya yamekuwa ukweli hivi karibuni. Katika mwaka uliopita pekee, kumekuwa na ongezeko kubwa la maslahi ya sarafu-fiche, kuboreshwa kwa ufumbuzi wa safu ya 2, majaribio makubwa ya aina mpya za utawala na mapinduzi katika utambulisho wa kidijitali.

Tuko mwanzoni tu wa kuunda Wavuti bora na Web3, lakini tunapoendelea kuboresha miundombinu ambayo itaiunga mkono, mustakabali wa Wavuti unaonekana mzuri.

Ninawezaje kushiriki

Masomo zaidi

Web3 haijafafanuliwa kwa ukali. Washiriki mbalimbali wa jumuiya wana mitazamo tofauti juu yake. ''Hapa kuna baadhi yao.'':

Pima uelewaji wako wa Ethereum

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 24 Februari 2026

Je! makala haya yamekusaidia?