
Jiunge na jamii
Karibu kwenye Kitovu cha Jamii ya Wana Ethereum
Jamii ya wana Ethereum ni mji wa mamia kwa maelfu ya wasanidi programu, wanateknolijia, wabunifu, watumiaji wawekezaji na wapenzi wa Ethereum.
Kwanini ujihusishe?
Tafuta jabila lako
Kuna kabila kwa ajili ya kila mmoja.
Jipatie riziki
Kila mmoja ana bili za kulipa. Ethereum hukuruhusu kujipatia kazi zenye maana, na kulipwa vizuri kuzifanya kazi hizo.
Tengeneza utofauti
Kushiriki katika Ethereum hukuruhusu kua mwenkezaji alie hai kwenye teknolijia yenye matokea chanya kwa mamilini ya watu.
Nawezaje kujihusisha?
Kuna njia nyingi za kujihususha na jamii ya Ethereum inayokua kwa kasi; unaweza kujiunga kwenye jamii mashuhuri za mtandaoni, shiriki kwenye kongamano, jiunge na mikutano, changia kwenye mdahalo au shiriki kwenye moja kati ya vikao vingi vya mtandaoni vya Ethereum.


Jiunge na jamii ya mtandaoni
Pata kabila lako na shiriki katika jamii na wapenzi wengine wa Ethereum.

Matukio ya Ethereum
Pata na shiriki kwenye mikutano ya Ethereum, au hackathon.

Changia kwenye mradi
Tupa jicho kwenye orodha ya namna za kushiriki ambazo unaweza kuchangia kulingana na ujuzi ulionao na taaluma yako.

Tafuta ruzuku
Utoaji wa ruzuku hukusaidia wewe kuinua pendekezo lako.
Muundaji? Mjenzi? Jipatie kipato kwa kazi yako.
Je unajenga juu ya Ethereum, ama unataka? Makampuni yanaajiri maelfu ya wataalamu wa kiufundi na wasio mafundi. Una pendekezo lako pekee? Jaribu kutafuta ruzuku ili kuanza kushughulikia wazo lako.

Changia kwenye ethereum.org
Kwa watu wengi, ethereum.org ndio hatua yao ya kwanza ya kujihusisha na ikolojia ya Ethereum. Inasasoshwa na kusahihishwa na maelfu ya wachangiaji wa vyanzo-vilivyo-wazi. Unataka kusaidia? Soma mwongozo juu ya uchangiaji, au weka suala kwenye GitHub.

Msaada wa Ethereum
Unahitaji msaada? Hakuna msaada rasni wa Ethereum, ila kuna mamia ya jamii ya wana-ethereum zinazoweza kukusaidia uweze kujiendeleza juu ya Ethereum.
