Nini ni NFTs?
NFT ni tokeni ambazo ni za kipekee kivyake. Kila NFT ina sifa tofauti (haziwezi kubadilishwa) na ni chache. Hii ni tofauti na tokeni kama vile au tokeni zingine zinazotumia Ethereum kama vile USDC ambapo kila tokeni inafanana na ina sifa sawa ('fungible'). Hutojali ni noti gani ya dola (au ETH) unayo kwenye pochi lako, kwa sababu zote zinafanana na zina thamani sawa. Hata hivyo, wewe unajali ni NFT gani maalum unayomiliki, kwa sababu zote zina sifa za kibinafsi zinazozitofautisha na zingine ('non-fungible').
Upekee wa kila NFT ni kuwezesha ishara ya vitu kama sanaa, vitu vinavyokusanywa ama mali isiyohamishika, ambapo kila NFT huwakilisha ulimwengu halisi ama bidhaa ya kidijitali. Umiliki wa rasilimali unaweza kuthibitishwa hadharani kwenye ya Ethereum.
Mtandao wa rasilimali
Tokeni zisizoweza kuigwa na Ethereum husuluhisha shida zinazokuwepo kwenye mtandao leo. Kwa kuwa kila kitu kinakuwa cha kidijitali, kuna haja ya kuiga sifa za vitu halisi kama uhaba, upekee na ushahidi wa umiliki kwa njia ambayo umiliki audhibitiwi na shirika la kati. Kwa mfano, ukiwa na NFTs unaweza kumiliki faili la muziki wa mp3 kupitia programu mahususi kwa ajili ya Ethereum na isiyo shikana na kampuni ya aina yoyote ya muziki kama Spotify au Apple music. Unaweza kumiliki jina la mtandao wa kijamii ambalo unaweza kuuza au kubadilisha, lakini haliwezi kuchukuliwa kutoka kwako kiholela na mtoa huduma wa jukwaa.
Hivi ndivyo mtandao wa NFT unafanya kazi ukilinganisha na mtandao ambao wengi wengi tunatumia leo...
Mlinganisho
| Mtandao wa NFT | Intaneti ya leo |
|---|---|
| Unamiliki rasilimali zako! Ni wewe tu unaweza kuziuza au kuzibadilisha. | Unakodisha rasilimali kutoka kwa shirika fulani na inaweza kuchukuliwa kutoka kwako. |
| NFTs ni za kipekee kidijitali, hakuna NFT mbili zinazofanana. | Mara nyingi nakala haiwezi kutofautishwa na ile ya asili. |
| Umiliki wa NFT huhifadhiwa kwenye blockchain ili mtu yeyote aweze kuthibitisha hadharani. | Upatikanaji wa rekodi za umiliki wa vitu vya kidijitali unadhibitiwa na taasisi – ni lazima uwaamini wanachosema. |
| NFT ni kwenye Ethereum. Hii inamaanisha zinaweza kutumika kwa urahisi katika mikataba-erevu mingine na programu kwenye Ethereum! | Kampuni zilizo na bidhaa za kidijitali kwa kawaida huhitaji miundombinu yao wenyewe ya "bustani iliyozungushiwa ukuta". |
| Waumbaji wa maudhui wanaweza kuuza kazi zao popote na wanaweza kufikia soko la kimataifa. | Waundaji wanategemea miundombinu na usambazaji wa majukwaa wanayotumia. Hizi mara nyingi hutegemea masharti ya matumizi na vikwazo vya kijiografia. |
| Waumbaji wa NFT wanaweza kubaki na haki za umiliki juu ya kazi zao wenyewe, na kuweka mirabaha ya programu moja kwa moja kwenye mkataba wa NFT. | Majukwaa, kama vile huduma za kutiririsha muziki, hubaki na faida kubwa zaidi kutokana na mauzo. |
NFT zinatumika kufanya nini?
NFT hutumika kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:
- kuthibitisha kwamba ulihudhuria tukio
- kuthibitisha kwamba ulimaliza kozi
- umiliki wa vitu vya michezo
- sanaa ya kidigitali
- kugeuza mali za kidunia kuwa tokeni
- kuthibitisha utambulisho wako kwenye mtandao
- kuzuia ufikiaji wa maudhui
- ukataji tiketi
- majina ya kikoa kwenye intaneti iliyogatuliwa
- dhamana katika
Labda wewe ni msanii amabaye angependa kushiriki kazi yake kupitia NFT bila wewe kupoteza udhibiti ama kuwapa waamuzi faida zako. Wewe unaweza kutengeneza mkataba mpya na kuweka bayana hesabu ya NFT, vipengele vyao na kiungo chao kwa kazi mahususi ya sanaa. Kama msanii, unaweza kupanga mirabaha utakayolipwa kwenye mkataba-erevu (k.m., hamisha 5% ya bei ya mauzo kwa mmiliki wa mkataba kila wakati NFT inapohamishwa). Unaweza pia kuthibitisha kila wakati kuwa umeunda NFT kwa sababu unamiliki uliotumia mkataba. Wanunuzi wako wanaweza kuthibitisha kwa urahisi kuwa wanamiliki NFT halisi kutoka kwa mkusanyiko wako kwa sababu ya mkoba wao inahusishwa na tokeni katika mkataba-erevu wako. Wanaweza kuitumia katika mfumo wa ikologia ya Ethereum, inayoaminika kwa uhalisi wake.
Ama zingatia tiketi ya tukio ya mechi ijayo. Kama vile mratibu wa tukio anavyoweza kuchagua ni tiketi ngapi za kuuza, muumbaji wa NFT anaweza kuamua ni nakala ngapi zitakuwepo. Wakati mwingine huwa na nakala za ziada, kama vile Tiketi 5000 za Kiingilio cha Jumla. Wakati mwingine nyingine zinachapishwa zinazofanana, ila kila moja ina tofauti ndogo na yenzake, kama vile tiketi yeneye nambari ya kiti. Hizi zinaweza kununuliwa na kuuzwa kutoka kwa mshirika mmoja mpaka kwa mwingine kusipokuwepo na ulipaji wa washikaji tiketi na wanunuzi watakuwa na uhakika wa tiketi halisi kwa kuangalia anwani ya mkataba huo.
Katika ethereum.org, NFTs hutumika kuonyesha kwamba watu wamechangia kwa dhati kwenye hazina yetu ya GitHub (wamepanga tovuti, wameandika au kurekebisha makala...), wametafsiri maudhui yetu, au wamehudhuria simu zetu za jumuiya, na hata tuna jina letu la kikoa la NFT. Ukichangia ethereum.org, unaweza kudai NFT. Mikutano mingine ya sarafu za kidijitali imetumia POAPs kama tiketi. Zaidi kuhusu kuchangia.
Tovuti hii pia ina jina mbadala la kikoa linaloendeshwa na NFT, ethereum.eth. Anwani yetu ya .org inasimamiwa na mtoa huduma wa mfumo wa majina ya kikoa (DNS), ambapo ethereum.eth imesajiliwa kwenye Ethereum kupitia Huduma ya Majina ya Ethereum (ENS). Na hii linamilikiwa na kuendeshwa na sisi. Angalia rekodi yetu ya ENS (opens in a new tab)
Zaidi kuhusu ENS (opens in a new tab)
NFT zinafanyaje kazi?
NFT, kama bidhaa zozote za kidijitali kwenye mnyororo wa bloku wa Ethereum, zinaundwa kupitia programu maalum ya kompyuta inyotegemea Ethereum, inayoitwa "mkataba erevu". Mikataba hii hufuata sheria fulani, kama vile viwango vya au , ambavyo huamua kile ambacho mkataba unaweza kufanya.
Mikataba erevu ya NFT zinaweza kufanya vitu vichache:
- Unda NFTs: Inaweza kutengeneza NFTs mpya.
- Gawa Umiliki: Hufuatilia ni nani anamiliki NFT zipi kwa kuzihusisha na anwani maalum za Ethereum.
- Ipe Kila NFT Kitambulisho: Kila NFT ina namba inayoifanya kuwa ya kipekee. Cha ziada, kikawaida kuna kuwa na baadhi ya taarifa (metadata) zinazo ambatanishwa nayo, inaelezea kitu kinachoiwakilisha tokeni isiyojirudia.
Wakati mtu "anatengeneza" au "kuunda" NFT, kimsingi wanaiambia mkataba erevu kuwapa wao umiliki wa NFT husika. Taarifa hii inalindwa kwa usalama na kuhifadiwa na umma kwenye blockchain.
Zaidi, muundaji wa mkataba anaweza ongeza sheria nyingine za ziada. Wanaweza dhibiti kiasi cha NFT kuweza kuundwa au kuamaua kwamba wanaweza pata ada ya mrabaha pale ambapo NFT inabadilisha mmiliki.
Usalama wa NFT
Usalama wa Ethereum unatokana na . Mfumo huu umebuniwa ili uweze kuondoa vitendo ya kihasidi kiuchumi na basi kuifanya Ethereum sugu kwa uharibifu. Hii ndiyo inayofanya NFT kuwezekana. Pindi chenye muamala wako wa NFT itamgharimu mshambulizi mamilioni ya ETH kukibadilisha. Mtu yeyote anayetumia programu ya Ethereum anaweza kujua haraka mambo yasiyofaa ya kuhitilafiana na NFT, na mtu huyu mbaya atatozwa malipo na kuondolewa.
Maswala ya usalama yanayohusiana na NFT sana sana yanahusiana na utapeli wa kutumia barua pepe, hatari za mkataba-erevu au makosa ya mtumiaji (kama vile kuweka wazi funguo za siri) na hivyo kufanya usalam bora wa pochi uwe muhimu sana kwa wamiliki NFT.
Zaidi kuhusu usalamaMasomo zaidi
- Mwongozo wa wanaoanza kuhusu NFTs (opens in a new tab) – Linda Xie, Januari 2020
- Kifuatiliaji cha NFT cha Etherscan (opens in a new tab)
- Kifuatiliaji cha NFT cha Blockscout (opens in a new tab)
- Kiwango cha tokeni cha ERC-721
- Kiwango cha tokeni cha ERC-1155
- Programu na Zana Maarufu za NFT (opens in a new tab)
Rasilimali zingine
Pima uelewaji wako wa Ethereum
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 16 Februari 2026

